Mlengo wa serikali siyo
sahihi
Nilizaliwa Tanzania, na niliondoka kuja USA zaidi ya miaka thelathini iliyopita, wakati nilikuwa
miaka ishirini. Tangu wakati huo, nimerudi Dare-es-salaam mara chache kuonana
na jamaa and marafiki. Safari yangu ya karibuni ya kuenda huko ilitokea baada
ya karibu miaka nane kutoka nilipoenda huko mwisho Juni 2006. Baada ya kusikia
sifa nyingi kuhusu maendeleo za Dar-es-salaam siku hizi, nilikuwa natarajia
kushangazwa kwa kizuri. Basi nilishangazwa kwa hakika, lakini siyo kwa kizuri.
Uandishi huu umekusudiwa kuongeza ufahamu kuhusu mambo ambazo zinaelekea
zinapuuzwa. Inatoa ukosoaji ya kizuri kuhusu, kwa maoni yangu, hali mbaya ya
mambo huko Dar-es-salaam, ikifuatiwa na mapendekezo maalum. Ni njia yangu ya
kufanya kitu kwa matumaini ya kuboresha hali hiyo.
Haichukui fikra kubwa kutambua kwamba miundombinu ya Dar-es-salaam hapo awali
ilibuniwa kwa idadi ya watu ambayo ilikuwa chini sana kuliko ilivyo sasa. Sababu kuu ya
kutokuelewana kati ya miundombinu na idadi ya watu, kwa maoni yangu, ni kwa
sababu Dar-es-salaam inakua zaidi kwa wima badala ya usawa.
Kwa mfano, pahala pengi ambapo miaka thelathini iliyopita kulikuwa na nyumba
zenye safu moja, sasa kuna miinuko mingi yenye viwango vingi - lawama zote ni
kwa watengenezaji wa majengo ambao wanaonekana wanalenga faida ya muda mfupi
dhidi ya gharama ya kuongeza mzigo wa maji, umeme, na maji taka juu ya
miundombinu zinayohusiana nazo. Matokeo yake, kwa bahati mbaya lakini kwa
kutarajiwa, ni matukio mengi ya maji taka kufurika barabarani. Hata mvua kidogo
kwenye hali kama hizo husababisha madimbwi makubwa ya maji machafu
kote mjini.
Lakini kuna uwezekano kwamba watengenezaji wa majengo (na yeyote ambaye
walilazimika kuhonga ili wapate vibali vya ujenzi, mikataba, nk) wamecheka njia
nzima mpaka benki. Na kuhakikisha kicheko chao ni ngumu sana, watengenezaji hao mara nyingi wanasisitiza kwamba
malipo zao ziwe kwa dola ya Amerika. Majaribio zao za kujitumikia, kwa maoni
yangu, sio mazuri kwa mji. Vivyo hivyo, wauzaji wa vifaa kama mapampu za maji, matangi ya kuhifadhia maji juu ya paa, na majenereta
za umeme pia wamecheka njia nzima hadi benki - ingawa vifaa hivyo vinatoa
suluhisho la muda mfupi tu kwa uhaba wa maji na umeme. Mbaya zaidi, vifaa kama hivyo haswa huzidisha shida ya maji taka kwa kusababisha uengezeko wa
matumizi ya maji. Inatubidi tukumbuke kwamba kusukuma maji safi juu kufika sakafu au eneo iliopo mbali ni kazi
rahisi. Changamoto ya kweli ipo kwenye kutafuta njia ya kutupa maji baada ya
kutumiwa na kuchafuliwa - yaani zaidi ya kuyaacha tu yaunde dimbwi na polepole
kuingia ndani ya ardhi.
Inaeleweka, miinuko nyingi mpya zilizojengwa zimesababisha uongezeko kubwa za
idadi ya watu mjini. Hiyo nayo imesababisha msongamano wa trafiki wa kutisha
kwenye barabara nyingi (mengi ambazo hazina alama za njia) karibu wakati wowote
wa kazi. Hiyo haishangazi kwani hizo barabara zinazohusika zilibuniwa
kushughulikia sehemu ndogo tu ya magari ambayo kwa sasa zinashughulikiwa.
Matumizi mabaya hayo ya barabara husababisha kutokea kwa mashimo makubwa ambayo
yanazidisha msongamano wa magari - haswa yanapojazwa na maji ya mvua
yaliyochanganywa na maji taka.
Watu wanaonekana kuwa na wakati zaidi huko, lakini hawaonekani kuwa na uwezo wa
kufanikiwa sana - lawama zaidi iende kwa msongamano wa trafiki ya
kutisha. Ilinichukua masaa mawili na nusu kufika uwanja wa ndege kutoka
Kariakoo tu. Hiyo pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watu na gharama kubwa ya
maisha ikilinganishwa na mapato zimefanya maisha kuwa ya dhiki na ya
kutatanisha kwa wanaoishi wengi huko. Hufanya mtu kushangaa ni vipi wauzaji
wengi wa matunda na mboga wanaishi kwa mapato yao ambayo yanaonekana chache bila kufanya shughuli
haramu. Hali mbaya kama hiyo huko labda inaelezea kwanini, wakati huu,
marafiki na jamaa wengi wanaoishi huko walionekana kuwa na wasiwasi na wasio na
urafiki.
Inadhaniwa, serikali inafanya kitu kukabiliana na hali hiyo ngumu ya kuishi.
Lakini kwa maoni yangu, mlengo wa serikali siyo sahihi kwa maana kwamba
rasilimali zinatumika katika shughuli ambazo zinaweza kufanya hali kuwa mbaya
zaidi - wakati wachache (kama watengenezaji wa mali na wauzaji wa vifaa
waliotajwa hapo awali) wanaendelea kujitajirisha na kuwaacha raia wakilala
nyuma.
Kwa mfano, sioni vipi ujenzi wa Bus Rapid Transit, uwanja wa ndege mpya wa
kimataifa, na daraja huko Kigamboni zimepewa kipaumbele taratibu katika juhudi
hizi, wakati miundombinu za maji, umeme, na maji taka zinahitajika kuboreshwa.
Bila shaka, juhudi zilizotajwa zitaongeza mtiririko wa watu kupitia mjini na
zitazidisha matumizi za miundombinu ambazo ni dhaifu hata sasa.
Fedha za serikali pia zimetumika kukusanya wauzaji wadogo wa barabarani na
kutowaruhusu kufanya biashara. Hoja, inaonekana, ni kuboresha hisia ya mji. Kwa
kukosekana na njia zingine za kujitafutia riziki, kuna uwezekano juhudi kama hizo potofu za serikali zitaongeza uwizi na ujambazi.
Nadhani rasilimali za serikali zingetumika vizuri zaidi ikiwa zingetumika
kuboresha mifumo ya umeme na maji taka. Au kuongeza ufahamu kwa umma juu ya
kutotupa takataka kwenye mifereji ya maji ya mvua. Au kuweka mapipa mengi ya
takataka kote mjini na kuweka ratiba thabiti ya kuchukua taka. Vivyo hivyo,
rasilimali za serikali zingetumika vizuri zaidi ikiwa zingetumika kukuza
ufahamisho wa madereva haswa wakati wapo kwenye msongamano wa magari. Nakumbuka
haswa dereva aliyesimamisha gari lake na hakuturuhusu kugeuka kulia (hata ingawa kulikuwa na
nafasi nyingi nyuma ya gari lake) ili tuweze kuharakisha mtiririko wa trafiki
upande wote. Kwa kukosekana kwa adabu ya kawaida ya kuendesha magari, hata
ujenzi wa njia za kupita kwa juu pale palipokwepo trafiki nyingi haitaweza
kupunguza msongamano wa magari.
Mara nyingi, niliona wafanyakazi wengi wakifagia kwa mikono mitaa ziliyojaa na
trafiki ili waondoe mchanga na vipande za ardhi - wakati huo huo, kulikuwa na
eneo la ardhi tupu na uchafu siyo mbali kutoka hapo. Natarajia mwajiri wao
alishinda zabuni ya kufanya shughuli kama hizo (zisizo na
maana, kwa maoni yangu) na alikuwa analipwa vyema kwa kutumia fedha za
serikali.
Ni kweli, hata wafanyikazi wa nyumbani na wauzaji wa mitaani Dar-es-salaam siku
hizi wana simu za mkononi, na waishi wa pale wengi wana iPads za hivi karibuni,
wanamiliki gari za bei ghali, na wanajua mambo mengi kuhusu mitandao ya
kijamii. Hoteli zingine hata zina helipad kuwezesha usafirishaji wa wateja
wenye shuguli nyingi kwa helikopta hadi uwanja wa ndege. Lakini, kwa maoni
yangu, hiyo haifanyi mji kusemeka imesonga mbele. Badala yake, hiyo inaimanisha
kwamba watengenezaji wengine (wa kigeni) wamejipatia soko kubwa la kuuza bidhaa
zao. Ningependa kuona rasilimali za serikali zikitumika kuendeleza fikra na
mitazamo ya wananchi, badala ya kuwapa tu ufikiaji wa vifaa vya kisasa.
Rasilimali za serikali pia zingetumika vyema zaidi ikiwa zitatumika kukuza
mawazo ya kufanya kazi kwa haki, kwa mfano, kutii ishara za trafiki, kufuata
maagizo ya askari wa trafiki, na sio kutupa taka taka hovyo hovyo. Vivyo hivyo,
pesa hizo zingetumika vizuri zaidi ikiwa zingetumika kuunda mazingira ambayo
polisi na polisi wa trafiki wanaonekana kama marafiki kuliko maadui. Mwagizo kubwa, najua - lakini sio lazima iwe
haiwezekani kufanyika.
Pamoja na mafikirio hayo, siwezi kuona jinsi mtu anavyoweza kuita mji
umeendelea ikiwa mawazo kawaida ya watu ni kwamba wezi, wakikamatwa, hupigwa au
huchomwa moto hadi wanakufa. Fedha za serikali zingetumika vizuri zaidi ikiwa
zingetumika kuleta uelewaji kwa umma kwamba mazoea hayo ni ya kinyama na
hayakubaliki kabisa katika karne ya 21. Ni jambo la kushangaza kwamba mawazo kama haya za kishenzi yanaendelea kushamiri Dar-es-salaam ingawa,
ikilinganishwa na miaka thelathini iliopita, kumekuwa na ongezeko kubwa la
idadi ya majumba za kidini na ibada.
Mwishowe, fedha za serikali zingetumika vyema zaidi ikiwa zingetumika kukuza
utumiaji wa hundi (na hata kadi za mkopo) badala ya pesa taslimu, kwani
matumizi zao zitaunda mazingira bora za kibiashara.
Ingawa ni rahisi kusema lakini ni ngumu kutekeleza kwa vitendo, rasilimali za
serikali zinabidi kupewa kipaumbele ipasavyo kwa nia ya kukuza mazoea na
mitazamo ambayo mwishowe zitawanufaisha wakaazi wote, sio wachache tu. Kwa
maneno mengine, kufanya jambo sahihi na kuwa na mawazo ya wote kushinda lazima
iwe msingi kuu ya kuendesha matumizi ya serikali. Ni matumaini yangu kwamba
aina ya ufahamu ambayo nakala hii imejaribu kukuza itakuwa na athari nzuri kwa
wote wanaohusika.
Ninatarajia kupata mshangazo wa kiwema wakati mwingine nitakapotembelea
Dar-es-salaam.
Nash Khatri
Julai 11, 2014