Sunday, January 10, 2021

Swahili version of my Nov 19, 2019 post "Long article sent in 2014 to Daily News Tanzania"

 

Mlengo wa serikali siyo sahihi


Nilizaliwa
Tanzania, na niliondoka kuja USA zaidi ya miaka thelathini iliyopita, wakati nilikuwa miaka ishirini. Tangu wakati huo, nimerudi Dare-es-salaam mara chache kuonana na jamaa and marafiki. Safari yangu ya karibuni ya kuenda huko ilitokea baada ya karibu miaka nane kutoka nilipoenda huko mwisho Juni 2006. Baada ya kusikia sifa nyingi kuhusu maendeleo za Dar-es-salaam siku hizi, nilikuwa natarajia kushangazwa kwa kizuri. Basi nilishangazwa kwa hakika, lakini siyo kwa kizuri. 

Uandishi huu umekusudiwa kuongeza ufahamu kuhusu mambo ambazo zinaelekea zinapuuzwa. Inatoa ukosoaji ya kizuri kuhusu, kwa maoni yangu, hali mbaya ya mambo huko Dar-es-salaam, ikifuatiwa na mapendekezo maalum. Ni njia yangu ya kufanya kitu kwa matumaini ya kuboresha hali hiyo.

Haichukui fikra kubwa kutambua kwamba miundombinu ya Dar-es-salaam hapo awali ilibuniwa kwa idadi ya watu ambayo ilikuwa chini
sana kuliko ilivyo sasa.  Sababu kuu ya kutokuelewana kati ya miundombinu na idadi ya watu, kwa maoni yangu, ni kwa sababu Dar-es-salaam inakua zaidi kwa wima badala ya usawa.

Kwa mfano, pahala pengi ambapo miaka thelathini iliyopita kulikuwa na nyumba zenye safu moja, sasa kuna miinuko mingi yenye viwango vingi - lawama zote ni kwa watengenezaji wa majengo ambao wanaonekana wanalenga faida ya muda mfupi dhidi ya gharama ya kuongeza mzigo wa maji, umeme, na maji taka juu ya miundombinu zinayohusiana nazo. Matokeo yake, kwa bahati mbaya lakini kwa kutarajiwa, ni matukio mengi ya maji taka kufurika barabarani. Hata mvua kidogo kwenye hali
kama hizo husababisha madimbwi makubwa ya maji machafu kote mjini.
 
Lakini kuna uwezekano kwamba watengenezaji wa majengo (na yeyote ambaye walilazimika kuhonga ili wapate vibali vya ujenzi, mikataba, nk) wamecheka njia nzima mpaka benki. Na kuhakikisha kicheko chao ni ngumu
sana, watengenezaji hao mara nyingi wanasisitiza kwamba malipo zao ziwe kwa dola ya Amerika. Majaribio zao za kujitumikia, kwa maoni yangu, sio mazuri kwa mji. Vivyo hivyo, wauzaji wa vifaa kama mapampu za maji, matangi ya kuhifadhia maji juu ya paa, na majenereta za umeme pia wamecheka njia nzima hadi benki - ingawa vifaa hivyo vinatoa suluhisho la muda mfupi tu kwa uhaba wa maji na umeme. Mbaya zaidi, vifaa kama hivyo haswa huzidisha shida ya maji taka kwa kusababisha uengezeko wa matumizi ya maji. Inatubidi tukumbuke kwamba kusukuma maji safi juu kufika sakafu au eneo iliopo mbali ni kazi rahisi. Changamoto ya kweli ipo kwenye kutafuta njia ya kutupa maji baada ya kutumiwa na kuchafuliwa - yaani zaidi ya kuyaacha tu yaunde dimbwi na polepole kuingia ndani ya ardhi.

Inaeleweka, miinuko nyingi mpya zilizojengwa zimesababisha uongezeko kubwa za idadi ya watu mjini. Hiyo nayo imesababisha msongamano wa trafiki wa kutisha kwenye barabara nyingi (mengi ambazo hazina alama za njia) karibu wakati wowote wa kazi. Hiyo haishangazi kwani hizo barabara zinazohusika zilibuniwa kushughulikia sehemu ndogo tu ya magari ambayo kwa sasa zinashughulikiwa. Matumizi mabaya hayo ya barabara husababisha kutokea kwa mashimo makubwa ambayo yanazidisha msongamano wa magari - haswa yanapojazwa na maji ya mvua yaliyochanganywa na maji taka.

Watu wanaonekana kuwa na wakati zaidi huko, lakini hawaonekani kuwa na uwezo wa kufanikiwa
sana - lawama zaidi iende kwa msongamano wa trafiki ya kutisha. Ilinichukua masaa mawili na nusu kufika uwanja wa ndege kutoka Kariakoo tu. Hiyo pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watu na gharama kubwa ya maisha ikilinganishwa na mapato zimefanya maisha kuwa ya dhiki na ya kutatanisha kwa wanaoishi wengi huko. Hufanya mtu kushangaa ni vipi wauzaji wengi wa matunda na mboga wanaishi kwa mapato yao ambayo yanaonekana chache bila kufanya shughuli haramu. Hali mbaya kama hiyo huko labda inaelezea kwanini, wakati huu, marafiki na jamaa wengi wanaoishi huko walionekana kuwa na wasiwasi na wasio na urafiki.

Inadhaniwa, serikali inafanya kitu kukabiliana na hali hiyo ngumu ya kuishi. Lakini kwa maoni yangu, mlengo wa serikali siyo sahihi  kwa maana kwamba rasilimali zinatumika katika shughuli ambazo zinaweza kufanya hali kuwa mbaya zaidi - wakati wachache (kama watengenezaji wa mali na wauzaji wa vifaa waliotajwa hapo awali) wanaendelea kujitajirisha na kuwaacha raia wakilala nyuma.

Kwa mfano, sioni vipi ujenzi wa Bus Rapid Transit, uwanja wa ndege mpya wa kimataifa, na daraja huko Kigamboni zimepewa kipaumbele taratibu katika juhudi hizi, wakati miundombinu za maji, umeme, na maji taka zinahitajika kuboreshwa. Bila shaka, juhudi zilizotajwa zitaongeza mtiririko wa watu kupitia mjini na zitazidisha matumizi za miundombinu ambazo ni dhaifu hata sasa.

Fedha za serikali pia zimetumika kukusanya wauzaji wadogo wa barabarani na kutowaruhusu kufanya biashara. Hoja, inaonekana, ni kuboresha hisia ya mji. Kwa kukosekana na njia zingine za kujitafutia riziki, kuna uwezekano juhudi
kama hizo potofu za serikali zitaongeza uwizi na ujambazi.

Nadhani rasilimali za serikali zingetumika vizuri zaidi ikiwa zingetumika kuboresha mifumo ya umeme na maji taka. Au kuongeza ufahamu kwa umma juu ya kutotupa takataka kwenye mifereji ya maji ya mvua. Au kuweka mapipa mengi ya takataka kote mjini na kuweka ratiba thabiti ya kuchukua taka. Vivyo hivyo, rasilimali za serikali zingetumika vizuri zaidi ikiwa zingetumika kukuza ufahamisho wa madereva haswa wakati wapo kwenye msongamano wa magari. Nakumbuka haswa dereva aliyesimamisha gari
lake na hakuturuhusu kugeuka kulia (hata ingawa kulikuwa na nafasi nyingi nyuma ya gari lake) ili tuweze kuharakisha mtiririko wa trafiki upande wote. Kwa kukosekana kwa adabu ya kawaida ya kuendesha magari, hata ujenzi wa njia za kupita kwa juu pale palipokwepo trafiki nyingi haitaweza kupunguza msongamano wa magari.

Mara nyingi, niliona wafanyakazi wengi wakifagia kwa mikono mitaa ziliyojaa na trafiki ili waondoe mchanga na vipande za ardhi - wakati huo huo, kulikuwa na eneo la ardhi tupu na uchafu siyo mbali kutoka hapo. Natarajia mwajiri wao alishinda zabuni ya kufanya shughuli
kama hizo (zisizo na maana, kwa maoni yangu) na alikuwa analipwa vyema kwa kutumia fedha za serikali.

Ni kweli, hata wafanyikazi wa nyumbani na wauzaji wa mitaani Dar-es-salaam siku hizi wana simu za mkononi, na waishi wa pale wengi wana iPads za hivi karibuni, wanamiliki gari za bei ghali, na wanajua mambo mengi kuhusu mitandao ya kijamii. Hoteli zingine hata zina helipad kuwezesha usafirishaji wa wateja wenye shuguli nyingi kwa helikopta hadi uwanja wa ndege. Lakini, kwa maoni yangu, hiyo haifanyi mji kusemeka imesonga mbele. Badala yake, hiyo inaimanisha kwamba watengenezaji wengine (wa kigeni) wamejipatia soko kubwa la kuuza bidhaa zao. Ningependa kuona rasilimali za serikali zikitumika kuendeleza fikra na mitazamo ya wananchi, badala ya kuwapa tu ufikiaji wa vifaa vya kisasa.
  
Rasilimali za serikali pia zingetumika vyema zaidi ikiwa zitatumika kukuza mawazo ya kufanya kazi kwa haki, kwa mfano, kutii ishara za trafiki, kufuata maagizo ya askari wa trafiki, na sio kutupa taka taka hovyo hovyo. Vivyo hivyo, pesa hizo zingetumika vizuri zaidi ikiwa zingetumika kuunda mazingira ambayo polisi na polisi wa trafiki wanaonekana
kama marafiki kuliko maadui. Mwagizo kubwa, najua - lakini sio lazima iwe haiwezekani kufanyika.
 
Pamoja na mafikirio hayo, siwezi kuona jinsi mtu anavyoweza kuita mji umeendelea ikiwa mawazo kawaida ya watu ni kwamba wezi, wakikamatwa, hupigwa au huchomwa moto hadi wanakufa. Fedha za serikali zingetumika vizuri zaidi ikiwa zingetumika kuleta uelewaji kwa umma kwamba mazoea hayo ni ya kinyama na hayakubaliki kabisa katika karne ya 21. Ni jambo la kushangaza kwamba mawazo
kama haya za kishenzi yanaendelea kushamiri Dar-es-salaam ingawa, ikilinganishwa na miaka thelathini iliopita, kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya majumba za kidini na ibada. 

Mwishowe, fedha za serikali zingetumika vyema zaidi ikiwa zingetumika kukuza utumiaji wa hundi (na hata kadi za mkopo) badala ya pesa taslimu, kwani matumizi zao zitaunda mazingira bora za kibiashara.
 
Ingawa ni rahisi kusema lakini ni ngumu kutekeleza kwa vitendo, rasilimali za serikali zinabidi kupewa kipaumbele ipasavyo kwa nia ya kukuza mazoea na mitazamo ambayo mwishowe zitawanufaisha wakaazi wote, sio wachache tu. Kwa maneno mengine, kufanya jambo sahihi na kuwa na mawazo ya wote kushinda lazima iwe msingi kuu ya kuendesha matumizi ya serikali. Ni matumaini yangu kwamba aina ya ufahamu ambayo nakala hii imejaribu kukuza itakuwa na athari nzuri kwa wote wanaohusika.

Ninatarajia kupata mshangazo wa kiwema wakati mwingine nitakapotembelea Dar-es-salaam. 

Nash Khatri

Julai 11, 2014